Monday, June 25, 2012

SISI TUTAIJENGA TANGA

Kufuatia ujenzi wa barabara ya Segera- Tanga, baadhi ya Wadau wametoa maoni yao kuhusu ubovu uliokuwepo katika barabara hiyo na huu unaoendelea katika barabara ya kutokea Himo-Segera. Barabara hiyo ni mbovu na imekuwa ikimeguka kila kukicha, kwa wengi walio wagonjwa hasa ambao magonjwa yao hayaendani na ubovu wa barabara wamekuwa wakihoji ni lini itapatiwa ufumbuzi angalau wa kuziba viraka tu. Tuanze kuwakumbusha Wabunge wetu juu ya ahadi zao walizozitoa kipindi kile cha kampeni kuhusu barabara zetu kwani inaonekana kidogo wameanza kujisahau.
Posting from an internet training with journalists in Arusha, Tanzania, 2010