Tuesday, February 22, 2011

MUAFAKA WA JANGA HILI NI LINI?

Poleni sana ndugu zetu Wahanga wa Mabomu huko Jijini, kwa mara nyingine tena janga la mabomu limeendelea kutesa familia lukuki katika nchi yetu.

Hivi ni kweli Wananchi tutakuwa na makosa gain pindi tutakapohoji kuhusiana na mauaji haya yasiyo na kificho kwa ndugu zetu? Naomba mnisaidie mimi kwa upeo wangu huu mdogo kuhusiana na hili….

Bado tuko pembezoni mwa ulimwengu huu tukiangalia na kutegesha macho na masikio yetu japo tupate kusikia kauli nzuri zitakazoturidhisha kwa hili ….Hivi ni kweli inawezekana kuwa ni bahati mbaya au ni Rehema ya Mungu kwamba yeye aliyeimba nchi na Dunia ndiye hasa anayesababisha kulipuka kwa mabomu Ardhini?

Naomba mnisaidie hili kwani kwa sasa walio wengi kama mimi tunasubiri tena kwa mara ya tatu kusikia kama ni zamu ya Mabibo au wapi…….

Kwa tahadhari za namna hii itakuwa saf sana kwani watu wanaweza kujiandaa kuhama makazi yao kwa hiari kuliko kuendelea kusubiria vifo visivyotamanika…….NATOA POLE YA DHATI KABISA KWA NDUGU WOTE WA MAREHEMU NA WALIOATHIRIKA NAMI NIKIWA MMOJAWAO..